Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mhe Batilda Burian akiongea na Watanzania waishio nchini humo mara tu baada ya kutoka kuwasilisha hati za utambulisho kwa Mfalme Akihito
Showing posts with label Tanzanite Society Japan. Show all posts
Showing posts with label Tanzanite Society Japan. Show all posts
Friday, July 10, 2015
Thursday, May 14, 2015
WATANZANIA NCHINI JAPAN WASHEHEREKEA MUUNGANO NA KUMUAGA MHE BALOZI SALOME SIJAONA
Sherehe ya Muungano na Kumuaga Mhe Balozi Salome Sijaona iliyofanyka April 26, 2015 katika ubalozi wa Tanzania Nchini Japan uliopo Setagaya, Tokyo nchini Japan
Mhe Balozi Salome Sijaona akipokea zawadi
Friday, July 20, 2012
SALAAM ZA RAMBI-RAMBI KUTOKA JAPAN
Meli iliyo zama - Picha na Nathan Chiume
Kwa niaba
ya Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan naomba
niwajulishe kwamba tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya
ajali ya meli ya MV SKAGIT,
iliyokuwa
ikisafiri kutoka Dar kuelekea Zanzibar, ambayo imesababisha wenzetu wengi
kupoteza
maisha na
wengine kujeruhiwa.
Tunawapongeza na kuwashukuru taasisi mbali-mbali na watu binafsi
wanaofanya kazi kubwa kukabili
zoezi la
uokoaji, na wale waliotufikishia habari hizi. Tunawashukuru wale wote waliopata
taarifa na
kuelekea
kwenye eneo la tukio na kuanza uokoaji mara moja.
Uongozi
wa Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan, tuko pamoja
nanyi,
na pia
tunaungana na Watanzania wenzetu wote kutoa pole kwa wafiwa, na kuwaombea
majeruhi waweze
kupona
kwa haraka. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote
na
kuwapa
nguvu na uvumulivu ndugu na jamaa, katika kipindi hiki
kigumu.
NJENGA,
Rashid
Mwenyekiti,
Jumuiya ya
Watanzania Waishio nchini Japan.
Subscribe to:
Posts (Atom)




.jpg)