Friday, July 20, 2012

SALAAM ZA RAMBI-RAMBI KUTOKA JAPAN‏


Meli iliyo zama - Picha na Nathan Chiume


Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan naomba
niwajulishe kwamba tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya meli ya MV SKAGIT,
iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar kuelekea Zanzibar, ambayo imesababisha wenzetu wengi kupoteza
maisha na wengine kujeruhiwa.

Tunawapongeza na kuwashukuru taasisi mbali-mbali na watu binafsi wanaofanya kazi kubwa kukabili
zoezi la uokoaji, na wale waliotufikishia habari hizi. Tunawashukuru wale wote waliopata taarifa na
kuelekea kwenye eneo la tukio na kuanza uokoaji mara moja.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan, tuko pamoja nanyi,
na pia tunaungana na Watanzania wenzetu wote kutoa pole kwa wafiwa, na kuwaombea majeruhi waweze
kupona kwa haraka. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote na
kuwapa nguvu na uvumulivu ndugu na jamaa, katika kipindi hiki kigumu.

NJENGA, Rashid

Mwenyekiti,
Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Japan.

No comments: