Saturday, December 05, 2009
TANZANITE SOCIETY JP
Tangazo la Mkutano (TANZANITE SOCIETY)
Ndugu Wanajumuiya wa TANZANITE society,Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Tanzanitesociety) napenda kuwataarifu kuwa, kutakuwa na mkutano mkuu wa Wanajumuiya wote utakaofanyika:Siku: Jumapili 6/12/2009Mahali (Ukumbi): Odasaga plaza (Odakyu sagamihara station)Muda: Kuanzia saa 12:15 jioniAgenda za mkutano huu ni kama zifuatazo:(1) Kupata taarifa mbalimbali za maendeleo ya Jumuiya (i.e Kuisajili Jumuiya kuwa NGO).(2) Kujadili na kutathmini zoezi la ulipaji ada kwa Wanajumuiya.(3) Kujadili na kuamua kuhusu kutenga fedha kusaidia wenye shida nyumbani Tanzania.(4) Maoni na mengineyo.Uongozi wa jumuiya unapenda kuwakumbusha kuwa, kama tulivyokubaliana katika mkutano uliopita, kwa wale wote watakaochelewa kufika kwenye mkutano au wasiofika bila kutoa taarifa kwa uongozi watatozwa fine.Mkutano utaanza rasmi saa 12:15 jioni, tunaomba kuzingatia muda.Taarifa za kutoweza kufika kwenye mkutano zipelekwe kwa Katibu Mkuu waJumuiya :Katibu mkuu: Julius MombekiSimu: 090 4130 4754Email: jullius57@docomo.ne.jp(NB) Pia kwa wale wote ambao sio wanachama(Wanajumuiya) hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mkutano.
Natanguliza shukrani,
E. Senkoro
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya.
Friday, November 27, 2009
Saturday, November 21, 2009
Friday, November 20, 2009
Tanzanite Society JP
Tangazo la Mkutano (TANZANITE SOCIETY)
Ndugu Wanajumuiya wa TANZANITE society,
Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Tanzanitesociety) napenda kuwataarifu kuwa, kutakuwa na mkutano mkuu wa Wanajumuiya wote utakaofanyika:
Siku: Jumapili 6/12/2009
Mahali (Ukumbi): Odasaga plaza (Odakyu sagamihara station)
Muda: Kuanzia saa 12:15 jioni
Agenda za mkutano huu ni kama zifuatazo:
(1) Kupata taarifa mbalimbali za maendeleo ya Jumuiya (i.e Kuisajili Jumuiya kuwa NGO).
(2) Kujadili na kutathmini zoezi la ulipaji ada kwa Wanajumuiya.
(3) Kujadili na kuamua kuhusu kutenga fedha kusaidia wenye shida nyumbani Tanzania.
(4) Maoni na mengineyo.
Uongozi wa jumuiya unapenda kuwakumbusha kuwa, kama tulivyokubaliana katika mkutano uliopita, kwa wale wote watakaochelewa kufika kwenye mkutano au wasiofika bila kutoa taarifa kwa uongozi watatozwa fine.
Mkutano utaanza rasmi saa 12:15 jioni, tunaomba kuzingatia muda.
Taarifa za kutoweza kufika kwenye mkutano zipelekwe kwa Katibu Mkuu wa
Jumuiya :
Katibu mkuu: Julius Mombeki
Simu: 090 4130 4754
Email: jullius57@docomo.ne.jp
(NB) Pia kwa wale wote ambao sio wanachama(Wanajumuiya) hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mkutano.
Natanguliza shukrani,
E. Senkoro
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya.
Mshale

“Wapenzi Wa Muziki kaeni Mkao Wa Kula, MSHALE msanii mpya anakuja kuwashika na Single yake Makini iitwayo NIWE NAWE, Karibuni. Pini Hili Limerekodiwa Pale Fish Crab ,chini ya Producer Mahiri, LAMAR. Ndani Ya Single Hii Mshale Amemshirikisha Rapper Maarufu katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, ambaye Jina Lake Limehifadhiwa Kwanza Mpaka Single hii Itakapoenda Redioni mapema wiki ijayo. Karibu MSHALE ndani ya Jukwaa la Bongo Fleva!”
Sunday, November 01, 2009
WAVUTI.COM

Da Subi anapenda kuwataarifu wasomaji kuwa tovuti ya mpya ya WAVUTI.COM imechukua nafasi ya iliyokuwa NUKTA77.COM na nukta77.blogspot.com Naomba yeyote aliyekuwa ameweka linki ya nukta77 aihariri na kuweka wavuti.com
Karibuni sana kutembelea kwa taarifa za nafasi za masomo na kazi kwa burudani na bila kusahau habari na porojo!Asanteni.wavuti.com
Tuesday, October 13, 2009
Michango ya Jumuiya
Ndugu wanachama wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani. Uongozi wa Jumuiya kwa mara nyingine tena unapenda kuwakumbusha wale wote ambao hawajalipa michango yao ya mwaka jana kufanya hivyo haraka iwezekanavyo. Tarehe ya mwisho kwa wale wasiolipa michango hiyo ni October 18, 2009. Lakini pia wanajumuiya hawa wanatakiwa pia kuendelea kulipa michango yao ya mwaka mpya wa fedha ya kuanzia mwezi wa nane 2009.
1. Kwa wale ambao wanatakiwa kulipa lakini wanasababu za msingi za kushindwa kufanya hivyo wanaombwa kwa mara nyingine kuwasiliana na viongozi kuwasilisha sababu zao.
2. Pia tunapenda kuwakumbusha wale waliomaliza michango yao ya mwaka uliopita kuwa, mwaka mpya wa fedha umeanza tangu mwezi wa nane, hivyo wasiolipa michango yao wafanye hivyo haraka iwezekanavyo.
3. Ni jukumu la kila mmoja wetu kukumbuka kuwa tusipotoa michango yetu Jumuiya haitaweza kuwasaidia watakaopatwa na matatizo kwani hatuna chanzo kingine cha mapato.
Ahsanteni,
Jullius L.Mwombeki Junior - Katibu Mkuu
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society)
Monday, October 12, 2009
Sunday, October 11, 2009
DISCO LA HARAMBEE
Disco na Harambee ya Kuwachangia Bw Abuu Omary na Bi Tatu Bwela
Disco hilo litafanyika siku ya JUMAPILI ya Tarehe 11 Mwezi wa 10 katika ukumbi wa SAGAMINO TROPICAN PUB kuanzia SAA TATU usiku. Ukumbi upo karibu na kituo cha train cha Sagamino (Sotetsu line)
Kiingilio kitakuwa Yen 1,500. Kwa wale watakaotaka kuchangia zaidi siku hiyo kutakutakuwa na Daftari la Michango ukumbini. Mapato ya Disko hili watakabidhiwa Bw Abuu na Bi Tatu.
Kwa wale wenzetu wasio weza kufika siku hiyo na wanapenda kuwasaidia watanzania hawa wanaweza kuwasilisha michango yao kwa kiongozi yeyote yule wa Jumuiya au kutuma mchango wake kwenye akaunti ya Jumuiya ilipo hapo chini:
ACC. NAME: Tanzanite Society
REPRESENTATIVE: Simba Ally Yahaya
ACC No.: 7916169
BRANCH NAME: Kunitachi
BRANCH No.: 666
BANK NAME: Mistui Sumitomo
Kwa wale watakaotaka maelezo zaidi tafadhali wasiliana na
Mwenyekiti: 090-3899-0638
Katibu: 090-4130-4754
Kamati ya starehe: 080-3458-8786
Ahsanteni na karibuni wote
Simba
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.













