KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Showing posts with label rambi rambi. Show all posts
Showing posts with label rambi rambi. Show all posts

Tuesday, June 16, 2015

TANZIA







Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba amefariki dunia leo katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.
Akithibisha kutokea kwa kifo hico, Kaimu Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Mh Mary Nagu amesema msiba huo umetokea leo asubuhi na kwamba marehemu alikuwa akisumbulia na kisukari na shinikizo la moyo kwa muda mrefu.
Mh. Nagu amesema serikali inaungana na waislamu wote kuomboleza msiba huo, na kumuelezea marehemu kwamba alikuwa ni kiungo muhimu kati ya waislamu na serikali.
Amesema taratibu nyingine zinashughulikiwa na Baraza la Waisilamu Tanzania BAKWATA ambao watatoa taarifa rasmi muda wowote hii leo
‪#‎RIPShabanSimba‬ Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajiun

Friday, July 20, 2012

RAMBI RAMBI KUTOKA UJERUMANI‏



UMOJA WA WATANZANIA  UJERUMANI (UTU)

UNATOA MKONO WA POLE NA RAMBI RAMBI KWA NDUGU NA JAMAA WALIOPATWA NA MAAFA KUTOKANA NA AJALI YA MELI  MV SKAGIT ILIYOTOKEA ENEO LA CHUMBE  ZANZIBAR SIKU YA TAREHE 18.07.2012.

UMOJA WA WATANZANIA NCHINI UJERUMANI UMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA TAARIFA ZA AJALI MBAYA AMBAYO IMESABABISHA VIFO.
UMOJA WA WATANZANIA UNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE NCHINI KATIKA KIPINDI HICHI CHA  MAOMBOLEZO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA 
MUNGU UBALIKI UMOJA WA KITAIFA

  MFUNDO PETER MFUNDO
          MWENYEKITI WA
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU)