Tuesday, June 16, 2015

TANZIASheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba amefariki dunia leo katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.
Akithibisha kutokea kwa kifo hico, Kaimu Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Mh Mary Nagu amesema msiba huo umetokea leo asubuhi na kwamba marehemu alikuwa akisumbulia na kisukari na shinikizo la moyo kwa muda mrefu.
Mh. Nagu amesema serikali inaungana na waislamu wote kuomboleza msiba huo, na kumuelezea marehemu kwamba alikuwa ni kiungo muhimu kati ya waislamu na serikali.
Amesema taratibu nyingine zinashughulikiwa na Baraza la Waisilamu Tanzania BAKWATA ambao watatoa taarifa rasmi muda wowote hii leo
‪#‎RIPShabanSimba‬ Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajiun

No comments: