Tuesday, May 11, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

Tafrija ya kumuaga Bw Maleko na Kumkaribisha Mh Balozi

Ndugu Watanzania kwa ujumla,

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani inapenda kuwatangaza kuwa kutafanyika tafrija ndogo ya kumuaga Ofisa Ubalozi Bw Maleko na pia kumkaribisha rasmi Balozi wetu Mpya Mh. Mama Salome Sijaona. Sherehe hiyo itafanyika siku ya tarehe 30/5/2010 (Jumapili), kuanzia saa kumi jioni mpaka saa mbili usiku katika ukumbi wa Tsuruma.Taarifa ya jinsi ya kufika kwenye ukumbi itatolewa baadaye

Bw Maleko ambaye tumekuwa naye kwa muda mrefu sasa amemaliza muda wake wake na tarejea nyumba siku za hivi karibuni. Bw Maleko licha ya kuwa mwanachama wetu hai, pia amekuwa karibu sana na watanzania katika shughuli mbalimbali za shida na sherehe.

Hivyo itakuwa vizuri watanzania wote wakapata muda wa kumuaga. Pia kama mnavyofahamu,
Balozi mpya wa Tanzania hapa Japani amewasili takribani miezi miwili na wengi wetu bado
hawajapata fursa ya kukutana naye. Hivyo basi siku hiyo itakuwa muafaka kwetu kukutana naye na kubadirishana naye mawazo na ikibidi kupata nahasa zake kuhusu mambo mbalimbali.

Lakini pia tungependa siku hiyo itumike kuwakutanisha watanzania ili nao waweze kubadirishana mawazo na kufahamiana ili kuweza kujenga umoja wenye nguvu zaidi.

Ingawa shughuli hii inaandaliwa na Jumuiya, Watanzania wote wanakaribishwa kuhudhuria pamoja na familia zao.

Ili kurahisisha shughuli za maandalizi, kama chakula na vinywaji, tunaomba wale wote watakaotaka kuhudhuria kuandikisha majina yao kwa kwa viongozi wafutao.

1. Abby senkoro: mail ewsenkoro@yahoo. com, Simu:090-9801- 4433
2. Juma Kipaya:080-3414- 4460
3. Upendo Mwimbage:080- 1326-9700
4. Mariam Yazawa:090-4422- 8555
5. Yasir Kiluke:090-4203- 3340
6. Bagilo Jumbe:090-1733- 7447
7. Amani Paul: mail: amani.paul@gmail. com, simu:080-4200- 0684

Siku ya mwisho ya kujiandikisha ni tarehe 22/5/2010. Pia tunaomba kusisitiza kuwa wale ambao hawatajiandikisha majina yao hawataruhusiwa kuingia ukumbini siku ya tafrija. Na wale watakaohudhuria wanatakiwa kuelewa kuwa ukumbi umekodiwa mwisho saa 2 kamili usiku hivyo tunawaomba wafike kwa muda unaotakiwa. Kulikuwa na tatizo la watu kuja bila kujiandikisha na kuchelewa kufika wakati tulipokutana na waziri mkuu na kupelekea shughuli ile kukatishwa katikati. Tusingependa hali hii ijirudie.

Karibuni wote

Uongozi

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani

No comments: