
Mtanzania, Karateka Yassir Kiluke mwenye shati jeupe atashiriki kwenye mashindano ya Karate yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Keio Plaza Hotel huko Hachioji kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni siku ya tarehe 23 Agosti 2009.
Keio Plaza Hotel iko kiasi cha dakika mbili kutoka kituo cha treni cha Hachioji.
2 comments:
Nikiwa ni mdau sugu wa blogu yako, nakushukuru kwa taarifa unazoleta kuhusu shughuli za Watanzania huko Japani. Kila la heri.
Hapa ni mahala tunapojumuika kujua yanayojiri upande wa Japan na hasa kwa waTanzania waishio na wajishughulishao na mambo mbalimbali huko.
Na sasa waendeleza kwa kutuunganisha na Kaka Yassir Kiluke. Twamtakia mpambano mwema hiyo kesho na twaamini atafanikisha ndoto zake
Nawe twakushukuru na twakutakia kila lililo jema
Post a Comment