Wednesday, March 11, 2015

TANZANITE SOCIETY JP - UJIO WA WAZIRI MKUU MH MIZENGO PINDANdugu watanzania,

Napenda kuwataatifu kuwa waziri mkuu wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo  Pinda anatarajiwa kuwa Japan kwenye kwenye Mkutano wa kimataifa huko Sendai.

Mheshimiwa waziri Mkuu akiwa katika ziara hiyo fupi, amependelea kuutana na watanzania waishio Japan. Hivyo basi, tunategemea kuwa na Mkutano na waziri mkuu tarehe 17 Machi 2015 pale kwenye ukumbi wa Ubalozi kuanzia saa kumi na moja jioni.

Naomba kwa wale watakaoweza kuhudhuria Mkutano huu watufahamishe kupitia mtandao huu au email ya Ubalozi (fmossongo@tanzaniaembassy.or.jp) ili tuweze kujua idadi ya watu watakaohudhuria. Tunahitaji kujua idadi ya wahudhuriaji kwa ajili ya matayarisho. Naomba siku ya mwisho ya kuidhinisha iwe ijumaa tarehe 13 Machi 2015.

Asanteni sana na jioni njema.

David P. Semiono
Mwenyekiti 
Tanzanite Society


No comments: