Friday, March 20, 2015

Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni walipoliweka jiji la Stuttgart chini yao
Bendi Maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni usiku wa Jumamosi ya 14 Machi 2015 walifanikiwa kufanya  mavitu yao jukwaani na kuliweka jiji la Stuttgart,chini ya himaya na muziki wao.katika onyesho hilo la Africa Unite Party , ulinzi ulioandaliwa katika onyesho lakini kikosi kazi Ngoma Africa band kilikuwa "Fit on Fire" , walisindikizwa jukwaani na askari maalumu wa ujerumani,lakini cha kushangaza wanamuziki wenyewe walikuwa katika mavazi ya ubaya ubaya ! kwa kuwa sheria za ughaibuni zinawaruhusu kutinga na viwalo..kila nchi inautaratibu na sheria zake ,wadaku wanatonya kuwa
bendi hiyo maarufu ilikuwa na ujumbe sio kila anayevaa viwalo vya ubaya ubaya au wajeda ni mvunja amani au mpenda vita bali anaweza kuwa mpiga gitaa badala ya mtutu "Peace for All",washabiki wengine walidai kuwa Ngoma Africa band walikuwa wanawachimbia mkwala baadhi ya vijana wa kijerumani 'Neo Nazi" wenye tabia za kuvamia wageni ambao pamoja na kuwapo ulinzi katika onyesho lile lakini labda wangeweza kupenyaNo comments: