Monday, March 25, 2013

TANGAZO LA MKUTANO WA WATANZANIA WOTE WAISHIO JAPAN

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tokyo, Japan, unapenda kuwatangazia Watanzania Wote waishio Japan kuwa, Mhe. Salome T. Sijaona, Balozi wa Tanzania Japan, atakuwa na Mkutano wa pamoja wa Watanzania wote tarehe 28 Aprili 2013 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi kuanzia saa 8:00 mchana.

Pamoja na mambo mengine mkutano utajadili yafuatayo:-

1. Ujio wa viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania katika mkutano wa TICADV (5th Tokyo International Conference for Africa Development) tarehe 1-3 Juni 2013,
2. Mikakati ya Watanzania waishio Japan katika kusukuma maendeleo ya Tanzania,
3. Taarifa nyinginezo:-

l Maoni ya Katiba
l Vitambulisho vya taifa,
l N.K

Anuani ya ukumbi wa Mkutano ni kama ifuatavyo:-

21-9 Kamiyoga, 4 Chome, Setagaya-Ku,Tokyo, 158-0098
Simu: 03-3425-4531, Nukushi: 03-3425-7844

Tafadhali thibitisha ushiriki wako kupitia anuani za barua pepe zifuatazo:-

tzrepjp@tanzaniaembassy.or.jp, tzrepjp@gol.com
jmaleko@tanzaniaembassy.or.jp,fmossongo@tanzaniaembassy.or.jp

Upatapo ujumbe huu tafadhali mjulishe na mwenzako.

Tangazo hili limetolewa na Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tokyo, Japan
26/03/2013
__._,_.___

No comments: