Sunday, April 29, 2012

SHUKURANI


KWA NIABA YETU NA KWA NIABA YA FAMILIA NZIMA YA MZEE NJENGA (MAREHEMU). TUNAOMBA KUCHUKUA NAFASI HII KUWASHUKURU WOTE AMBAO WAMEKUWA NASI KWA NAMNA MBALIMBALI TANGU KUMUUGUZA MZEE WETU MPAKA ALIPOTUTOKA.

TUNAWASHUKURU WOTE WALIOTUTUMIA UJUMBE, WALIOTUPA RAMBI-RAMBI ZAO, NA WALE AMBAO WAMETUTUMIA JUMBE KUPITIA EMAILS NA WENGINE WALIOTUPIGIA SIMU KUTUPA POLE MARA TU WALIPOPATA TAARIFA YA MSIBA. KWA KWELI JUMBE ZENU TUMEZISOMA ZOTE NENO KWA NENO, MSTARI KWA MSTARI NA ZIMETUFARIJI SANA.

TUNAWASHUKURU WOTE WALIOACHA SHUGULI ZAO MUHIMU NA KUAMUA KUJUMUIKA NASI SIKU YA TAREHE 15/ APRIL/2012 KWA AJILI YA KUFANYA MAOMBI, NA KUTUPA RAMBI RAMBI ZAO, KULE SAGAMIHARA. MARA TULIPOREJEA KUTOKA NYUMBANI. BAADHI YENU MLIPATA TAARIFA YA MUDA MFUPI TU, LAKINI MLIWEZA KUSHIRIKI PAMOJA NASI.

TUNAWASHUKURU WALIOTUSAIDIA KU-ORGANIZE MKUSANYIKO ULE, WALIOTUPA PAHALA PA KUKUSANYIKIA, WALIOTUSADIA KWA UPANDE UANDAAJI WA CHAKULA N.K.

SHUKRANI MAALUM ZIUENDEE UBALOZI WETU HAPA TOKYO KWA KUWA KARIBU NASI NA MAOFISA WAKE AMBAO WAMESHIRIKIANA NASI KWA KARIBU NA WAMEHUDHURIA MAOMBI.

NI VIGUMU KUMTAJA KILA MMOJA NA NAMNA AMBAVYO AMESHIRIKIANA NASI. TUNAWAOMBA WANGINE WOTE AMBAO HATUKUWAGUSIA KWENYE UJUMBE HUU MTUWIE RADHI NA MPOKEE SHUKRANI ZETU ZA DHATI KABISA.

NI VIGUMU PIA KUPATA MANENO AU MAELEZO SAHIHI YANATOSHA KUELEZEA KINA CHA SHUKRANI ZETU KWENU. TUNAOMBA MPOKEE MAELEZO YETU HAPA JUU KAMA KIELELEZI AU KIWAKILISHI CHA KINA CHA SHUKRANI ZETU PAMOJA NA SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA ZETU.

ASANTENI SANA.

ABBU NA RASHID NJENGA.
JAPAN

No comments: