Monday, July 04, 2011

khangazzz!!!3 comments:

Mbele said...

Mumyhery mimi nakufagilia sana, nikitumia lugha ya vijiweni. Tangu zamani ninafuatilia shughuli zako kwa mtazamo huo.

Ujasiriamali unaofanya, wa kuuza bidhaa (kwako hizi ni kanga) kutoka Tanzania, ndio haswa unaotakiwa. Unawapa au kudumisha ajira za watu kule nyumbani na unaliingizia Taifa fedha za kigeni.

Tanzania inahitaji kuuza bidhaa zake nje. Hilo ni suala ambalo halihitaji utaalam mkubwa wa uchumi. Na kuna masuala mengine rahisi ya namna hiyo, lakini ya msingi, kwa ajili ya kulinusuru Taifa letu. Nimeyaelezea hayo katika kitabu cha CHANGAMOTO. Tatizo ni kuwa ukiwa na jambo, ukaliandikia kitabu, watu wa Hii Nji (jina kapuni) hawataliona.

Cha zaidi ni kuwa ninavyoangalia shughuli zako naona wazi kabisa kuwa wewe ni balozi makini wa nchi yetu na utamaduni wake. Hongera sana, na nakutakia kila la heri.

emu-three said...

Hilii lingependekezwa na kuitwa `vazi la wanawake wa kiafrika!

Swahili na Waswahili said...

Kanga nzuri dada Mumyhery, kuna kanga moja hapo zamani waliita jicho lang'ombe IMETULIA WANGU!!!!!!!!!