Thursday, May 19, 2011

Tanzanite SocietyNdugu Wanajumuiya na Watanzania wote kwa ujumla,

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani unapenda kuwatangazia kuwa kutakuwepo na Mkutano wa wanajumuiya wote na Watanzania wote. Agenda za Mkutano ni kama zilivyoorodheshwa hapo chini.

Lakini kikubwa ni kufanya uchaguzi ili kujaza nafasi za Uongozi zilizopo wazi pamoja na kumuaga Mwenyekiti Mstaafu, Dr. Simba.

Uongozi unaomba mahudhurio yenu. Tafadhali fika katika Ukumbi wa Ubalozini kama ifuatavyo :

1. Siku: 22 Mei 2011 (Jumapili)
2. Muda: Saa 9 (Tisa) jioni hadi saa 1 (moja) usiku
3. Mahali / Sehemu : Ukumbi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Tokyo Japani.
4. Ajenda:

(1) Kufungua Mkutano- Kaimu Mwenyekiti.
(2) Kufanya Uchaguzi Mdogo
(3) Kutoa/Kupokea michango ya mwezi kutoka kwa wanachama. Kupokea wanachama wapya.
(4) Mengineyo.
(5) Nasaha kutoka kwa Balozi, Balozi kufungua rasmi sherehe ya kumuaga M/kiti Mstaafu.
(6) Kumuaga Mwenyekiti Mstaafu, Dr. Simba.

5. Jinsi ya kufika Ubalozini:
http://www.tanzaniaembassy.or.jp/english/TheEmbassyinJapan/workinghours_en.html

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Jullius L. Mwombeki Jnr
Katibu Mkuu
Jumuiya ya WaTanzania Wanaoishi nchini Japani

No comments: