Tuesday, May 17, 2011

FFU wa Ngoma Africa Band jukwaani tena! 28-05-2011

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU
yenye maskani yake nchini ujerumani, inatazamiwa kutumbuiza katika maonesho ya
Afrika & Orient Festival,huko mjini Burg Satzvey jirani na miji ya Bonn na Koln,nchini
Ujerumani,siku ya jumamosi 28.Mai.2011 kuanzia saa 1.00 usiku.
Kamanda wa kikosi kazi hiko Ras Makunja wa FFU atakiongoza jukwaani kikosi machachari na
kuhakikisha kuwa gwaride la mziki linamfikia kila mshabiki..
bendi hiyo yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji wakiwemo wacharaza magitaa wakali kama
vile Chris-B,Said Jazbo Vuai,Maxime buanda..na wengineo,Ngoma Africa band pia maarufu kwa tabia
yao ya kuwadatisha akili na kuwatia kiwewe washabiki.
bendi hiyo imetajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyofanikiwa kuufanya muziki ndio daraja na urimbo
wa kuwanasa mamilioni ya wasahabiki katika kila kona duniani...
Ngoma Africa band ilianzishwa mwaka 1993 pia imetajwa na vianzo vingi vya habari kuwa ni bendi pekee ya kiafrika
hiliyo weza kuimiri vishindo vingi vya washabiki sugu barani ulaya..na kila wanapotumbuiza katika maonyesho ya kimataifa
wanakuwa na kazi moja tu... nayo ni kuhakikisha washabiki wanapagawa na kudata akili...
wasikilize zaidi
at www.reverbnation.com/ngomaafricaband
au www.myspace.com/thengomaafrica

jiunge nao at www.ngoma-africa.com
wasiliana nao contact@ngoma-africa.com

No comments: