KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Sunday, March 13, 2011

Tetemeko Japan




Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani , Bw. Francis Mussongo ametoa wito maalum kwa watanzania wanaoishi nchini Japani kuchukua hadhari kufuatia habari za kuvuja kwa mnunurisho wa nyuklia. Hii ni taarifa yake kamili;

Ndugu watanzania mliopo Japani

Kwa Mujibu wa taarifa zinaendelea kutolewa na NHK Japan, mitambo ya Nuclear Fukushima Plant (1) kuanzia saa 10 jioni kwa muda wa Japan inatoa radiations na kuna dalili za mlipuko katika kituo hicho, Hali hii imepelekea kutangazwa kwa hali ya dharura na watu wote wa maeneo hayo wanatangaziwa kuondoka maeneo ya karibu na eneo hilo ili kuepusha madhara endapo hali hii itaendelea. Endapo mlipuko utatokea kuna uwezekano wa kuleta madhara kwa watu na mali hadi umbali wa kilomita 10 kutoka eneo la Kinu hicho cha Nyuklia. Kwa kutambua kuwa kuna watanzania wenzetu katika eneo la Fukushima kupitia mtandao huu tunaomba wenye mawasiliano na wenzetu waliko Fukushima kuwajulisha kuondoka katika maeneo hayo. Tahadhari pia inatolewa pia maeneo ya Fukushima kuna uwezekano wa kutokea Tsunami tunashauri wenzetu waliko huko wajulishwe kuondoka maeneo ya ufukweni ili kujihami.

Francis Mossongo,
Afisa mwandamizi Ubalozi wa Tanzania,
Tokyo...12, March, 2011

Habari zilizo patikana hivi sasa zina sema kwamba watanzania wote wako salama hapa Japani...

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Tunamshukuru Mungu kwani mioyo ilikuwa hoi kabisa.

Mbele said...

Poleni sana. Mungu awanusuru.