Wednesday, March 09, 2011

Tanzania Society

Ndugu, Wanajumuiya pamoja na Watanzania wote mnaoishi Japan.

Naomba turejee kwenye taarifa iliyotolewa awali na Katibu Mkuu, nachukua nafasi hii tena kuwaarifu kuwa,
kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama Wote Siku ya Jumapili, Tarehe 20, Machi, 2011.

Mkutano huu utafanyika katika Ukumbi wa Odakyu Sagamihara Station (ODASAGA). Pale ambapo mikutano yetu hufanyika.
Mkutano utaanza saa 10, jioni na kumalizika saa 2, usiku (4:00pm - 8:00pm).

Mgeni Rasmi ni Ofisa kutoka Ubalozini, Mh. Mossongo

Agenda za Mkutano huu ni:
1. Kuhakiki Mapato na Matumizi ya Jumuiya Yetu
2. Kujaza nafasi zinazoachwa wazi na Mweka Hazina na Mwenyekiti Kamati ya Nidhamu
3. Tafrija fupi ya Kuwaaga Mweka Hazina Ndg. Juma Kipaya na Mwenyekiti Kamati ya Nidhamu, Ndg Amani Paul.
4. Mengineyo kwa idhini ya Mwenyekiti

Kuwapo kwa kila mmoja wetu katika Mkutano huu kutasaidia kufanikisha haya tunayoyakusudia kuyatimiza.

Tunawaomba wote muweke kumbukumbu kwenye ratiba zenu za siku hii ya Jumapili, tarehe 20, Machi, 2011.

Asanteni,

NJENGA, Rashid
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya
K.n.y Katibu Mkuu.

No comments: