Friday, March 04, 2011

Tanzania Society

Ndugu Wanajumuiya na Watanzania wote kwa ujumla,
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani unapenda kuwatangazia kuwa kutakuwepo na Mkutano mkuu kwa Wanajumuiya wote na Watanzania wote ambao utafanyika jumapili ya tarehe 20 March 2011.

Ajenda, mahali na wakati mara matayarisho yote yatakapo kamilika. Tunaomba yeyote yule mwenye hoja za kujadiliwa aziwakilishe kwa Katibu Mkuu au Makamu Katibu Mkuu ili ziwekwe kwenye ajenda za mkutano.

Naomba sote kwa ujumla tusaidiane kuwafahamisha wanajumuiya wote na wale ambao hawajafanya juhudi za kujiunga na jumuiya kuhusu mkutano huu muhimu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Jullius L. Mwombeki Jnr
Katibu Mkuu
Jumuiya ya WaTanzania Wanaoishi nchini Japani.

No comments: