KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Wednesday, March 16, 2011

TANZANIA HOUSE JAPAN



Ujumbe kwa Watanzania waishio Japan

Ubalozi wa Tanzania Japan unapenda kuwajulisha kuwa umeendelea kupokea taarifa kutoka mamlaka za Serikali ya Japan kuhusu hali inavyoendela kufuatia hitilafu ya mitambo/vinu vya kufua nuklia iliyotokea na inayoendelea kutokea katika mkoa wa Fukushima, pamoja na matetemeko yanayoendelea. Ubalozi umehakikishiwa kwamba bado maeneo mengi ni salama, ukiacha maeneo ambayo yapo umbali wa km 20 kutoka katika mitambo hiyo (exclusive zone) na km 20 hadi 30 ambako watu wamepewa maelekezo ya kukaa ndani.


Aidha, Ubalozi umejulishwa kuwa, pamoja na kwamba mionzi ya nuklia kutoka kwenye vinu hivyo imeweza kusambaa hadi maeneo mengine kama Tokyo, Kanagawa, Kawasaki, Ibaraki n.k., kiwango kilichopo ni kidogo sana kuweza kuleta madhara kwa afya ya binadamu.


Pamoja na taarifa hizo zilizotolewa na Serikali ya Japan kuwa hali ni salama, Ubalozi unawaomba Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari zaidi. Hivyo, unatoa rai kwa Watanzania wote wanaoishi Japan kutoa ushirikiano ili Ubalozi uweze kuweka rekodi zao kwa usahihi (up-date information), ukizingatia kwamba baadhi walisharudi Tanzania, wengine wamehamia katika maeneo mengine na wapo pia waliobadilisha namba zao za simu. Taarifa hizo zitausaidia Ubalozi kufanya mawasiliano ya haraka na kila mtu endapo hali ya kiusalama itakuwa mbaya na kulazimu tahadhari za ziada kuchukuliwa.


Hivyo tunaomba kila Mtanzania atume taarifa zifuatazo kwenye anwani za Ubalozi zitakazotajwa hapo chini.

1. Jina kamili
2. Orodha kamili ya familia yako (kama unaishi na familia)
3. Anwani ya mahali unapoishi (mtaa/mji/eneo n.k.)
4. Namba za simu unazotumia (mobile phone/residential)mawasiliano yake ikiwa ni pamoja na jina, simu/email, anuani ya napoishi, eno/mji/mtaa, n.k.


Taarifa hizo zitumwe kwenye e-mail addresses zifuatazo:-

Ubalozi unaomba ushirikiano wenu, na kila upatapo ujumbe huu tafadhali mjulishe na mwenzako.

Tafadhali tunaomba taarifa hizo zitumwe kwenye anuani pepe zifuatazo

1. jmaleko@tanzaniaembassy.or.jp
2. fmossongo@tanzaniaembassy.or,jp
3. tzrepjp@tanzaniaembassy.or.jp
4. tzrepjp@gol.com


Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania, Japan.

16/03/2011

1 comment:

emu-three said...

Twashukuru sana kwa taarifa hii poleni sana Watanzania mnaoishi huko!