Wednesday, March 16, 2011

baada ya tetemekoTetemeko lilipo isha tukabadili nguo tukisubiri usafiri, mara likatokea tetemeko lingine dogo wakati tunasubiri usafiri, nilipo lihisi tu nikawashitua wenzangu na kuanza kuwaambia jishin jishin jishin yaani tetemeko tetemeko tetemeko, tuaanza kutafuta mlango, wakataka kukimbila mlango wa mbali lakini mimi nikakumbuka kuna mlango pale karibu ndio nikaanza kuwaambia kokoo kokoo kokoo, hapa hapa hapa, walipo nifuata nikakumbuka tunakotaka kumbilia ngazi za huko zina machuma machuma ndipo nikawaambia stop bado tuna tafutana tetemeko likapungua tuka tulia ndivyo ilivyo kuwa matetemeko yalikuwa yanaendelea lakini madogo madogo, hivyo yakianza tunatafutana yakipungua tunatulia ikwa kama mchezo mwisho tukawa tunajicheka tu, mada aru mada aru, bado lipo bado lipo, warta warta warta limeisha limeisha limeisha , abunai hatari

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Hata kama sijaelewa kinachoongelewa namshukuru mwenyezi Mungu kuwa hali ipo salama kidogo.