KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Sunday, September 05, 2010

Futari

Ndizi Nyama




Vipimo
Ndizi mbichi 10
Nyama kilo 1
Nazi ya kopo 1
Chumvi 1 Kijiko cha chakula
Ndimu 1
Bizari ya manjano 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi 3
Nyanya (tomatoes) 2
Kitunguu maji 1
Thomu na Tangawizi ya kusaga 1 Kijiko cha chakula

Namna ya Kutayarisha Na Kupika
1. Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
2. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
3. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
4. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
5. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
6. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
7. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
8. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
9. Weka pembeni zipoe.
10. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

2 comments:

emu-three said...

Mhhh, sijui nije kwako kwa ajili ya futari leo, unaishi wapi Mummy!

mumyhery said...

emu3 karibu sana Hiratsuka