Saturday, July 10, 2010

SHYROSE BHANJI KUGOMBEA UBUNGE KINONDONI
Shy-Rose Bhanji ajitosa ubunge jimbo la Kinondoni· Asema mwaka 2010 ubunge unahitaji tafsiri mpya· Aainisha maeneo nane atayoyafanyia kazi· Kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana· abainisha umuhimu wa ofisi kila kata ndani ya jimboKada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji ametangaza kujitosa katika nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia CCM na lengo lake kubwa ni kuwa kiungo muhimu katika jamii ya wanakinondoni.Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Shy-Rose alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kabisa. `…kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo kama ilivyozoeleka` alifafanua Shy-Rose.`Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananch` alisema.Kwa maana hiyo amesema kwamba hata sifa za mbunge zinahitaji kutafsiriwa upya kabisa, kwani majukumu yake yamebadilika kuendana na wakati. Ametaja baadhi ya sifa hizo mpya ni kuwa mhamasishaji, kiungo muhimu, kufanya kazi usiku na mchana na kuwa na ofisi katika kila kata ndani ya jimbo husika ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.`naomba nitoe tafsiri mpya ya neno ubunge..mbunge anatakiwa sasa awe ni kiungo muhimu kati ya walio na kipato kikubwa, kipato cha kati na wasio na kipato kabisa ili kwa pamoja jimbo liweze kupiga hatua za kimaendeleo. Mimi nitahakikisha kwamba nina ofisi katika kila kata ili niweze kuwafikia wananchi wangu katika kata zote kwani wakati napita kuomba kura ninawafuata na baada ya kufanikiwa kutimiza azma yangu ni wakati wa kuendelea kuwafuata na si wao kunifuata` alisema.Kada huyo amesema sera yake kubwa itakuwa ni kumshirikisha kila mwananchi wa Kinondoni katika shughuli za kuleta maendeleo ili kila mtu aweze kutoa maoni, mawazo na mchango wa hali na mali katika kuleta maendeleo ya ukweli. Amesema hata mwananchi ambaye atakuwa hana uwezo, atabeba tofali kutoka upande mmoja hadi sehemu husika.`nimeamua kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge kwa jimbo la hili ili niweze kuleta mageuzi makubwa sana katika jimbo la Kinondoni…naomba mfahamu kwamba kila mwananchi amebarikiwa akili, vipaji uwezo na Mwenyezi Mungu lakini asiposhirikishwa hataweza kutoa mchango wake, hivyo mimi nitahakikisha kwamba kila mmoja kwa uwezo wake na nafasi yake anachangia katika kuleta maendeleo`, alifafanua.Shy-Rose alibainisha mambo makubwa ambayo atayapigania kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ni elimu, afya, ajira kwa vijana, kupiga vita utumiaji wa madawa ya kuleta kwa vijana, kupigania haki za wasanii, kusaidia wajane katika kujikwamua kiuchumi na kuleta msukumo mpya kabisa katika masuala ya mahusiano na jamii ambayo kwa mtazamo wake eneo hili linahitaji msukumo mpya.Shy-Rose amesema kwamba kutokana na uzoefu wa kazi zake tangu akiwa mwandishi wa habari, mtangazaji na Meneja uhusiano katika sehemu alizofanyia kazi, anaamini amekuwa mwanafunzi mzuri katika kutambua matatizo yanayoikabili nchi nzima na hususan na jimbo la Kinondoni

No comments: