Thursday, June 10, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

Kanto Summer PartyDJ Kidume

DJ Zee


DJ Simple K


Msanii Daima

Prof Abuu

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society inapenda kuchukuwa fursa hii
kuwatangazia Watanzania wote wa Kanto na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na sherehe kabambe ya
majira ya joto itafanyika huko Mkoani Kanagawa. Mgeni rasmi katika shughuli hii atakuwa Ofisa
Mwandamizi wa ubalozi Bw Maleko. Maelezo kamili ya shughuli hiyo ni kama ifuatavyo:-
Siku: 19/6/2010 (Jumamosi)
Muda: Kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo
Kiingilio: Yeni 1500 (utapata kinywaji kimoja)
Ukumbi: Sagimino BG Club. Dakika 1 toka kituo cha train cha Sagamino (Soutetsu line)

Ma-DJ na Wasanii: kutakuwana burudani toka kwa DJ mkongwe, DJ Zee, Pamoja na vijana wanaokuja
kwa kasi kubwa DJ Kidume pampoja na DJ Simple kutoka Chiba . Pia Yule Msanii machachari Mr Daima
kutoka Chiba atamalizia ile mistari aliyobakisha siku ya sherehe za kumkaribisha Mheshimiwa Balozi.
Usikose pia kuja kumuona Prof Abuu Jr akipiga mpini. Miziki ya aina mbalimbali kuanzia zile ya kizazi
cha zamani (enzi za mababu zetu) mpaka za kizazi kipya, hip hop, taarab, Reggae na itakuwepo.

Kwa ufafanuzi na maelekezo ya ziada tafadhali wasiliana na wafuatao:
Bi Upendo: 080-1326-9700
Bi Mariam: 090-4422-8555
Bw Kipaya: 080-3414-4460

Tunawaomba watanzania pamoja na marafiki zao wa mataifa mengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha
shughuli hii. Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.

Ahsante
Uongozi
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.

No comments: