Friday, March 12, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

UJIO WA WAZIRI MKUU WA TANZANIA NCHINI JAPANI

Ndugu Watanzanni wenzaguWaziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda anatarajia kuitembelea Japani kuanzia tarehe 24/3/2010 mpaka 27/3/2010.Mheshimiwa Waziri Mkuu anatarajia kukutana na waTanzania wanaoishi nchini Japani siku ya tarehe 26/3/2010 katika Hotel ya New Otani ya mjini Tokyo kuanzia mida ya saa 12 jioni.Ili kurahisisha zoezi la maandalizi ya mkutano huo basi, wale wote watakaoweza kuhudhuria wanaombwa kuwasilisha majina yao kwangu ili kupata idadi kamili ya wananchi watakaokuwepo.Majina haya au idadi hiyo inatakiwa kupatika kabla ya tarehe 17/3/2010.Unaweza kuwasiliana nami kwa njia zifuatazo:-Email: ayasi@yahoo.com Simu: 090-3899-0638. Tafadhali ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio ili naye aweze kuhudhuria.

Ahsanteni na natanguliza shukrani zangu za dhati

Ally Yahaya Simba
Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani

No comments: