Friday, November 20, 2009

Tanzanite Society JP

Tangazo la Mkutano (TANZANITE SOCIETY)

Ndugu Wanajumuiya wa TANZANITE society,
Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Tanzanitesociety) napenda kuwataarifu kuwa, kutakuwa na mkutano mkuu wa Wanajumuiya wote utakaofanyika:
Siku: Jumapili 6/12/2009
Mahali (Ukumbi): Odasaga plaza (Odakyu sagamihara station)
Muda: Kuanzia saa 12:15 jioni
Agenda za mkutano huu ni kama zifuatazo:
(1) Kupata taarifa mbalimbali za maendeleo ya Jumuiya (i.e Kuisajili Jumuiya kuwa NGO).
(2) Kujadili na kutathmini zoezi la ulipaji ada kwa Wanajumuiya.
(3) Kujadili na kuamua kuhusu kutenga fedha kusaidia wenye shida nyumbani Tanzania.
(4) Maoni na mengineyo.
Uongozi wa jumuiya unapenda kuwakumbusha kuwa, kama tulivyokubaliana katika mkutano uliopita, kwa wale wote watakaochelewa kufika kwenye mkutano au wasiofika bila kutoa taarifa kwa uongozi watatozwa fine.
Mkutano utaanza rasmi saa 12:15 jioni, tunaomba kuzingatia muda.
Taarifa za kutoweza kufika kwenye mkutano zipelekwe kwa Katibu Mkuu wa
Jumuiya :
Katibu mkuu: Julius Mombeki
Simu: 090 4130 4754
Email: jullius57@docomo.ne.jp
(NB) Pia kwa wale wote ambao sio wanachama(Wanajumuiya) hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mkutano.
Natanguliza shukrani,
E. Senkoro
Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya.

1 comment:

chib said...

Tangazo hilo la mkutano limenivutia.