Tuesday, October 13, 2009

Michango ya Jumuiya

Ndugu wanachama wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani. Uongozi wa Jumuiya kwa mara nyingine tena unapenda kuwakumbusha wale wote ambao hawajalipa michango yao ya mwaka jana kufanya hivyo haraka iwezekanavyo. Tarehe ya mwisho kwa wale wasiolipa michango hiyo ni October 18, 2009. Lakini pia wanajumuiya hawa wanatakiwa pia kuendelea kulipa michango yao ya mwaka mpya wa fedha ya kuanzia mwezi wa nane 2009.
1. Kwa wale ambao wanatakiwa kulipa lakini wanasababu za msingi za kushindwa kufanya hivyo wanaombwa kwa mara nyingine kuwasiliana na viongozi kuwasilisha sababu zao.
2. Pia tunapenda kuwakumbusha wale waliomaliza michango yao ya mwaka uliopita kuwa, mwaka mpya wa fedha umeanza tangu mwezi wa nane, hivyo wasiolipa michango yao wafanye hivyo haraka iwezekanavyo.
3. Ni jukumu la kila mmoja wetu kukumbuka kuwa tusipotoa michango yetu Jumuiya haitaweza kuwasaidia watakaopatwa na matatizo kwani hatuna chanzo kingine cha mapato.
Ahsanteni,
Jullius L.Mwombeki Junior - Katibu Mkuu
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society)

5 comments:

chib said...

Ni vizuri watu kuwa wanakumbuka kulipia michango badala ya kusubiri kukumbushwa, labda kama hawajui umuhimu wa jumuiya hizi.
Nawatakia kila la heri

Yasinta Ngonyani said...

taratibu nzuri mnazo!!

Yasinta Ngonyani said...

Dada M u mzima kwani ukimyao unanisibu:-)

mumyhery said...

Ahsante sana Chib

Yasinta, nimetingwa kidogo, na pilika za maisha, usiwe na wasi tuko pamoja

Yasinta Ngonyani said...

Poa , Nashukuru kama u mzima. pole na pilika pilika hizo. Tupo pamoja.