KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YETU, HAPA JAPAN
2011-11-19 06:04:56
Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Japan, Tanzanite, nachukua nafasi hii kuwaarifu kuwa tunaandaa tafrija kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru wa Nchi yetu, Tanzania. Tunakusudia kufanya tafrija kwa ufanisi zaidi ya ile iliyofanyika mwaka jana, kwa kuwa hii ni tafrija ya kusherehekea miaka 50. Ilikufanikisha shughuli hii tunaomba ushiriki wa kila mmoja wetu, kwa hali na mali.
Tunaomba mchango kutoka kwa kila mmoja wetu.
•Kima cha chini ni Yen 3,000; na ni ruksa kwa mtu kuchanga kiasi chochote kinachozidi hiki.
•Tunategemea kufanya tafrija hii Tarehe 17/Decemba/2011
Wakati na Mahala tutawatangazia.Kwa kuwa hatuna siku nyingi kufikia tarehe ya tafrija tumepanga Tarehe 30/Novemba/2011 kuwa ndiyo siku ya mwisho ya kupokea michango.
Kadi za mialiko zitatolewa kwa wale watakaochanga
Fresh Jumbe na kundi lake watatumbuiza katika tafrija hii.Ni wakati mzuri wa kukutana wote kwa pamoja, kula chakula, kupata vinyawaji na burudani huku tukitafakari yale tunayojifunza wakati huu tunaposherehekea Miaka 50.
Michango itumwe kwenye akaunti ifuatayo (ukiweza tupigie simu kutujulisha mchango wako, au tutumie barua pepe.
=================================
ACC. NAME: Tanzanite Society
REPRESENTATIVE: NJENGA, RASHID OMAR
ACC No.: 7916169
BRACH NAME: Kunitachi
BRANCH No.: 666
BANK NAME: Mitsui Sumitomo
No comments:
Post a Comment