Futari ya Pamoja
Jumuiya ya Waislam Nchini Japan yaandaa karamu ya futari ya Ramadhan Jumamosi tarehe 4th Sept 2010.
Lengo kuu la karamu hii ni kuwafanya Watanzania waishio hapa Japan kumkumbuka Mwenyeezi Mungu na kufanya mambo mema ambayo Mwenyeezi Mungu ameyasema ndani ya Quraan Tukufu. Pia kujenga mshikamano na upendo baina ya Watanzania waishio hapa Japan.
Katika karamu hii itasomwa Quraan Tukufu, waadhi, na dua na Masheikh mbali mbali.
Tunaomba Watu wote ambao wana elimu ya dini ya kiislam kujitokeza katika kutoa maada mbali mbali juu ya uislam.
Tunaomba Masheikh na Maalim wote watakao kuwa na waadhi au maada wajiandikishe kipitia kwa:-
1: Ahmed Maulid Tel No: 080 3150 9173
2: Ally Kanagawa Tel No: 080 5075 7879
Kufika sehemu husika wasiliana na Taji Nguku Tel No: 080 6563 7879
No comments:
Post a Comment