Muhogo wa Nazi na Samaki wa Kukaanga
Muhogo 3
Tui La Nazi 2 vikombe
Chumvi kiasi
Pilipili mbichi 2
Mafuta 1 kijiko moja
Kitunguu maji 1 kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
2. Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
3. Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
4. Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine.
source: http://www.alhidaaya.com/
2 comments:
Du! mate yamejaa mdomoni,umenitamanisha hii kitu natamani kama ningeweza kuupata muhogo leo na mimi ningepika kama ilivyo kwenye kwenye picha.....lkn naishia kula kwa ramani ya picha.
Hamna kama muhogo kwa karanga utakula mpaka kidole kwa utamu.
Post a Comment