
Summer Party/Nane Nane
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inapenda kuchukuwa fursa hii kuwatangazia Watanzania wote wa Kanto na maeneo ya jirani na wale watakaokuwa wanatembelea Kanto wakati huu wa kipindi cha majira ya joto kuwa kutakuwa na sherehe kabambe ya pamoja ya summer na kuadhimisha siku ya wakulima nyumbani Tanzania (Nane-Nane) siku ya tarehe 8/8/2009 huko Mkoani Kanagawa. Maelezo kamili ya shughuli hiyo ni kama ifuatavyo:-
Siku: 8/8/2009 (Jumamosi)
Muda: Kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo
Kiingilio: Yeni 1500 (utapata kinywaji kimoja)
Ukumbi: Tropican Pub (zamani Thaitech-Area51) Sagamino, dakika 5 toka kituo cha train cha Sagamino (sotetsu line):
Mengineyo: Muziki wa nguvu toka kwa DJ ZEE, Kumbuka DJ Zee ameshuka juzi toka mjini akiwa na box kubwa la CD za kila aina ya muziki, kuanzia zile za kizazi cha zamani (enzi za mababu zetu) mpaka za kizazi cha kipya.
Kwa ufafanuzi na maelekezo ya ziada tafadhali piga simu zifuatazo
Mwenyekiti Kamati ya Starehe(Pembe): 080-3458-8786
Wanakamati:
Bi Angela:080-3397-0339
Bi Upendo:080-1326-9700
Bi Mariam:090-4422-8555
Bw Ntale:080-3255-2210
Simu ya Ukumbi:046-778-0560
Uongozi wa Jumuiya unawaomba Watanzania pamoja na marafiki zao wa mataifa mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha sherehe hii. Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzako.
No comments:
Post a Comment