KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Sunday, July 26, 2009

The Tanzanite Band







Ndugu Watanzania wenzangu tuishio maeneo ya Tokyo,Saitama,Chiba,Kanagawa na kwingineko,napenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na burudani safi katika ukumbi wa Continental au kwa ndugu yetu bwana Daddy Mweli(kwa Daddy)siku ni ijumaa tarehe 31 Julai 2009,kuanzia saa 3.30(tatu na nusu)ya usiku,burudani hiyo italetwa na Bendi yetu mashuhuri ya ki Tanzania kama mnavyoijua kwa jina la The Tanzanites Band chini ya uongozi wa gwiji la muziki Fresh Jumbe Mkuu akishirikiana na Abbu Omar Prof.Jnr(gita) Lister Elia".com"Daudi Joseph,kaka Micky Jaga Jaga,bwana mdogo Amarido Kilinda.Bar hii ya Continental kwa wasiojua pahali ilipo ni stesheni iitwayo Soobudai Mae katika line ya Odakyu,treni hiyo huanzia Shinjuku hadi Sagamiono ,na hapo unaingia local treni hadi Soobudai Mae ni stesheni ya tatu kutoka Sagamiono,safari hii wana The Tanzanite Band wanaahidi kuwa watawasha moto mkali kushinda siku zote,Dr.Kamu, mweyekiti Dr. Simba na timu yenu msikose kuja kutupa tafu kama kawaida yenu tunategemea sapoti yenu,pia msisahau kuja na miswaki yenu maana siku hiyo ni mpaka chee!!!"minna san yoroshiku onegaishimasu"
ni mimi ndugu yenu mtiifu Abbu Omar(gita)Prof Jnr,Kwa niaba ya uongozi wa The Tanzanite Band Tokyo,asanteni .



No comments: