Watanzania wakutana kujadili yanayowahusu
Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania hapa Japani hivi leo Ijumaa jioni imeitisha kikao cha dharura kuwakutanisha Watanzania wachache kujadili kero mbalimbali zinazowakabili wananchi pamoja na tofauti zilizojitokeza hivi karibuni zilizochangia kutokuelewana miongoni mwa baadhi ya Watanzania wanaoishi hapa Japani. Kikao hicho kilikuwa chini ya Kaimu Balozi na kilihudhuriwa na maafisa wote waandamizi wa ubalozi. Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania nao walikuwepo kusaidia katika jitihada za kuondoa tofauti zilizojitokeza ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa Watanzania wanaoishi hapa Japani. Blogu ya jamii imepata picha chache za kikao hicho ambacho kilikuwa na mafanikio makubwa.

5 comments:
Tunawaombea heri na kikao kiwa na mafanikioa mema na kama kuna tofauti basi mziondoe
Jamani jipigeni moyo. Huku ughaibuni ni ugenini. Bora matatizo ya aina hiyo yatupate tunapokuwa Bongo, kwani kule kuna mtandao wa ndugu, jamaa, marafiki, na vijiwe vingi vya kupunguzia "stress." Huku ughaibuni kuna pia suala la utamaduni wa kigeni, ambalo linaweza kuyafanya matatizo yawe makubwa zaidi. Tunawatakieni heri na fanaka.
Tunashukuru kama kikao kilikuwa na mafanikio !
Natumaini kikao kilienda safi
hayaaa ndugu zetu wajapan kuna nini tena!naunga mkono wadau wote waliotoa comment.jameni sote ni ndugu nini tena kinatufanya tuwe tofauti nawatakia kila la kheri na natumai kumepatikana muaafaka.mungu wabarikiki watz wote walio japan na mueendelee kuwa na mshikamano kama wenzenu sehemu nyengine.
Post a Comment