KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Thursday, June 18, 2009

Jee Huu ni Uungwana?


Wenye makaratasi tuache kuwarudhisha wenzetu mjini




Abuu Gita


Jamani watanzania wenzangu hasa tunaoishi hapa Japan,tumekua na kamtindo ka kutishana kurudishana bongo,yaani wenye makaratasi(viza) kuwaripoti wasio na viza kwenye mamlaka husika yaani polisi nk.Inaonekana kukitokea tu kutoelewana baina yetu (hasa sisi watanzania)na siyo ndugu zetu raia wa nchi nyingine za ki afrika,tunaamua kuitiana polisi,kwa kweli huu si uungwana hata kidogo nami kwa asilimia mia moja napinga kabisa tabia hii ya kinyama,nadhani dugu zangu watanzania wenzangu mtaniunga mkono kwa kulipinga vikali swala hili na pia naomba ubalozi wetu wa Tanzania ufuatilie kwa karibu sana swala hili na wahusika katika matendo haya waadhibiwe vikali hata watengwe mbali na jumuia yetu ya watanzania tuishio hapa Japan,Kwa kawaida mimi huwa siandiki sana maoni yangu kwenye mtandao huu mimi huwa msomaji tu ila ikibidi niandike huandika.Nimeamua kutoa machungu yangu kutokana na kuitendo cha kinyama kilichofanywa na ndugu zetu au wadogo zetu wa kitanzania wasiokuwa na moyo wa kizalendo kwa kumpiga na kumjeruhi vibaya sana kaka yetu Saidi Mpemba na kumteka nyara hadi kituo cha Polisi cha Zama,na kumripoti kwa kumhisi kuwa anatembea na mwanamke wao wa kijapani!!,na kuwa hana vibali vya kuishi hapa ki halali hadi sasa tunavyozungumza huyu bwana Saidi bado anazuiliwa na polisi na huenda akakabidhiwa kwenye idara ya uhamiaji hapa Japan kama tujuavyo ukishafika kule na hali kama ya kaka Saidi ujue ndiyo safari ya nyumbani bila kupanga ,kama ulikuwa na madeni juu yako, kama ulikuwa na watu au familia inayokutegemea juu yako ,kama ulikuwa hujajenga kazi kwako je? huu ni uungwana?Kwa kawaida tangu zamani sisi watanzania tumekuwa na sifa za kuwa na heshima ,mapendo na mshikamano popote pale tulipo.kuanzia nyumbani hadi nchi za nje,kwa kifupi mimmi na wasanii wenzangu au wanamuziki wa kitanzania tumeishi hapa Japani kwa takribani miaka 15 sasa,na tulikuja hapa kwa ajili ya kazi yetu ya kisanii(proffesiona l musicians)kulingana na uzoefu wetu wa kuishi katika nchi hii tumekuwa na mapendo,umoja na mshikamano wa kweli na watnzania wenzetu,hadi miaka michache tu iliyopita ndipo maelewano(baadhi) ya watanzania wenzetu yakaanza kuwa mabaya,Nadhani bado hatujachelewa, tujaribu kusafisha uozo huu wa tabia zisizo za kistaarabu katika jamii yetu kabla mtu mwingine


hajarudishwa mjini??naomba huyu bro Said Mpemba awe wa mwisho na hawa mbwana wadogo wenye tabia mbaya waonywe vikali,kama kuna matatizo ya kutoelewana baina yetu ni vizuri kutumia uongozi wa jumuia yetu,au watu wenye uwezo wa kusuluhisha mambo,hata ikibidi ubalozi wetu mambo ya kihuni yamepitwa na wakati,Naomba ndugu yangu bwana Fresh Jumbe utoe maoni yako kuhusu swala hili nakumbuka mimi na wewe tumetoka mbali yaani tumefanya kazi hii ya muziki pamoja kwa miaka hii yote 15,na hatujawahi kuona watanzania wakisalitiana kama hivi sasa eti kwa ajili ya wanawake wa kijapani!!!ndugu yangu Lister Elia wewe pia tumotoka mbali pamoja katika kazi yetu hii hii,naomba maoni yako najua kuwa hatujawahi kurudisha mjini mtanzania yeyite na hatuta fanya jambo hilo asilan,Nyumbani ni nyumbani hakuna mtu asiyetaka kurudi bongo kwanza tuna miss sana nchi yetu tukufu ya asali na maziwa,ila kwenda bongo kunahitaji matayaridho na siyo ghafla namna hiyo TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE!!MUNGU IBARIKI TANZANIA Amen!!!!ni mimi Abbu Gita(Prof Jnr)

1 comment:

Anonymous said...

Duh poleni sana, kumbe hiyo tabia ya kijinga imefika mpaka huko??? nilidhani wanayo wapemba wa uk tuu?? yaani ni tabia mbovu sanaa mtu unamuharibia mwenzio maisha for stupid reason??? wats mwanamke??? halafu mwanamke mwenyewe wa kijapani asiyejua hata kujisafisha kunako?????. mimi siko huko na thank god nimesettle where i am. ila kama ingekua otherways mtu akinichomea nirudi bongo, Wallah ningefanya juu chini mpaka nahikikisha na yeye analost.
coz hali za bongo zenyewe tunajua tunaishi vp, leo mtu umepata visa umetoka bongo unafanya kazi inakupa senti mbili tatu mtu anirudishe?
Anyway jitahidini msikaribishe hiyo tabia ya kipumbavu hapo na watu wanaowachomea wenzao kama vp mnawafanyia umafia tuu.
coz akumulikae mchana usiku atakuchoma so kabla hajakuchoma wee mbanike.