KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Tuesday, July 15, 2008

Taarifa ya Mkutano

Ndugu watanzania wenzangu.
Kwa niaba ya Kamati ya kuandaa mkutano mkuu wa Watanzania kuchagua
viongozi wa kudumu.Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza nafasi
zitakazogombewa katika kipindi cha uchaguzi mkuu na sifa za mgombea.
1. Jumuiya itakuwa na viongozi wafuatao
(a) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
  (b) Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu.
  (c) Katibu Mwenezi.
  (d) Mweka Hazina na Naibu Mweka Hazina.
Pia jumuiya itakuwa na kamati mbili.
(i) Kamati ya Usuluhishi na Nidhamu.
(ii) Kamati ya Uhamasishaji, Starehe na Shida.
Kwa mujibu wa katiba kwa wale wote watakaopenda kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi((a)~(b)), watatakiwa kuwa na sifa zifuatazo.
2. Kiongozi wa Jumuiya awe na sifa zifuatazo:
(a) Awe Mtanzania.
(b) Awe ameishi nchini Japani sio chini ya miezi sita na awe anategemewa kuishi
nchini Japani kwa zaidi ya mwaka mmoja.
(c)Awe na uwezo wa kumudu nafasi ya uongozi anayopewa.

Mkutano utafanyika katika ukumbi wa Tsuruma siku ya Jumapili, tarehe 27 mwezi Julai
kuanzia saa 10 jioni. Anuani na ramani ya jinsi ya kufika ukumbi wa mkutano zitatolewa
baadaye.

★ Ndugu watanzania wenzangu, Kwa wale wote watakaopenda kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi wanaruhusiwa kuanza kampeni. Mgombea anaruhusiwa kutumia
njia ya mtandao kufanya kampeni(Kijinadi) .
Agenda kamili ya mkutano itasambazwa wiki moja kabla ya mkutano.
Natanguliza shukrani.
Senkoro.

1 comment:

Anonymous said...

Haya wenye sifa hizo jitokezeni ili 2pata kiongozi bora na sio bora kiongozi.
Habari ndio hiyo.