KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Saturday, July 18, 2015

MAGUFULI NDIYE MGOMBEA URAIS WA CCM 2015





MBUNGE wa Biharamulo Mashariki (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli ameshinda katika uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda baada ya kupata jumla ya kura 2104 sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali amepata kura 253 sawa na 10.5% na Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ndiye aliyepewa jukumu la kusoma mshindi katika kura za Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi mkoani Dodoma.















No comments: