Friday, March 20, 2015

KIONGOZI WA EXTRA BONGO BAND ALLY CHOKI KULITINGISHA JIJI LA TOKYO
APEWA MAPOKEZI MAZURI NA KUPANDA JUKWAANI NA WAKONGWE FRESH JUMBE NA ABBU OMARY  Mwanamuziki mahili wa muziki wa dansi Ally Choki ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya Extra Bongo aka "Wazee wa Kizigo" anatarajiwa kutingisha jukwaa siku ya Jumamosi 21.Machi 2015 ambapo wanamuziki wa Eagle's Vission watakuwepo kumsindikiza Ally Choki anayefuatana na Super Nyamwela.Katika onyesho hilo
wakongwe wawili wa muziki wa dansi watanzania wanaoishi Japan wanamuziki
Fresh Jumbe Mkuu na Abbu Omary watakuwepo jukwaani kuwapa baraka zote
wadogo zao Ally Choki na Super Nyamwela katika ukumbi wa Sehemu inaitwa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City pembeni kiduchu ya Jiji la Tokyo.

Madhumuni ya ziara ya Ally Choki na Super Nyamwela ni kuangalia ushirikiano na uwezekano wa soko la muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" ili muziki huo uweze kushika kasi kubwa na soko Japan na mashariki ya mbali kwa ujumla,Pia
uwezekano wa bendi ya Extra Bongo kufanya ziara za kimataifa. Wadau msikose
kujitokeza kwa wingi katika Onyesho hili waswahili usema 'Chereko Chereko na mwenye mwana"
No comments: