Sunday, February 22, 2015

TOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO Hiyo picha siyo ya Ksher....


INASIKITISHA SANA UKISOMA HII AMEANDIKA
K.SHER MSANII MWENYE ULEMAVU WA NGOZI
AKILIA JU YA ALBINO WANAVYO ULIWA TANZANIA
TAFADHAR SHARE KADRI UWEZAVYO ILIKUPINGA
UNYAMA HUU NA UJUMBE UFIKE KWA RAIS. 


Hata cjui niongee nini ila dah mmevuka mipaka
sasa hivi mh Rais Dr Jakaya Mrisho kikwete hivi ni
kweli hamuwajui wauwaji au?? Maana kila nikikaa
hainiingii akilini hivi hao wauwaji wana utaalam gani
wa serikali kushindwa kuwatia mkononi au mnataka
tuwafikirie nini jamani kwamba mbahusika au? Au
hii sio issue ya kitaifa mkaichukulia mkazo kama
mnavyochukulia zingine inaniuma sanaaaaaaa na
ninakata tamaa na nchi yangu kila siku zinavyozidi
kwenda natamani niiikimbie hii nchi niende mbali
ambapo labda sitoweza kushuhudia huu ukatili
unaoendelea ndani ya nchi mnayoiita nchi yenye
amani.maisha yetu yapo hatarini mh Raisi cjawahi
kujutia kuzaliwa hivi am always proud na nilivyo
lakini this time aahh ee mungu Nisamehe mja wako
kwa mara ya kwanza najutia kuwa na hii hali nikiwa
katika nchi mbovu kama hii mnayoiita nchi yenye
amani johana Rip mdogo wangu poleni sana familia
nzima ya mtoto Yohana sina nguvu ya kutetea zaidi
ya kuongea hisia zangu hapo nipo nipo
ninapotamani zaidi kuwa na nguvu katika serikali ili
niweze kutetea haki zetu by actions ngoja nisome
kwa bidii ili tukutane huko huko stop killing us
tuacheni tuwe katika nchi yetu.
SHARE UJUMBE HUU ILI KILA MTU AONE NA
MUNGU ATAKUBARIKI.
Note; Hiyo picha siyo ya Ksher.....

No comments: