Sunday, February 15, 2015

INAFRIKA BAND KUTOKA DAR WATINGISHA JIJI LA BREMEN,UJERUMANI
Inafrika Band aka Wazee wa Indege wakifunika bila ya huruma mjini Bremen,Ujerumani.
 Mashabiki wakifurahia onyesho la inafrika band.
Bendi ya muziki INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar ,ilifanikiwa kulitingisha jiji la Bremen,nchini Ujerumani katika onyesho liliofanyika usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa Musik-Theater mjini Bremen,Ujerumani,ambako bendi hiyo kutoka Chang'ombe ilisimama jukwaani na kuziteka nyoyo za maelfu ya wapenzi wa muziki ,aidha bendi ya Inafrika bend imetajwa kuwa bendi bora ya muziki wa Folk na radio Funkhaus-Europe .
Vionjo vya mitindo ya muziki wa asili wa makabila ya kitanzania vilivyotumiwa na Inafrika Band katika kuteka yonyo za washabiki kila kuona duniani. Inafrika Band imefanikiwa kuliweka jina la Tanzania katika tufe la dunia kwa kutumia mitindo yake ya vionjo vya kiasilia.
Inafrika Band ndio bendi kwanza yenye makao Tanzania inayoongoza kufanya tour ndefu duniani wameshafanya ziara katika mabara yote duniani kuanzia Afrika,Austaria,Amerika,Asia ,Europe na visiwa vya Karebiki.
Wakali hawa wa mdundo inayokubalika kimataifa wanatisha na kuzoa washabiki kwa dhoruba kali la mtindo wao wa muziki. Inafrika band inatuwakilisha bado wapo katika ziara ndefu na wanahakikisha kuwa muzikiwa wao unasikika kila kona nje ya mipaka ya kimataifa.

No comments: