Saturday, November 30, 2013

Tanzanite Society JP

Ndugu Watanzania,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa tutafanya kikao cha wanajumuiya wote wa Tanzanite. Pia wale ambao sio bado wanajumuiya na wangependa kufahamu zaidi kuhusu jumuiya hii wanakaribishwa.

Muda: 1 Desemba 2013 kuanzia saa kumi na moja jioni.
Mahali: Ukumbi wa Odasaga plaza ghorofa ya nne. (Odakyu Sagamihara Station).

Kati ya mada zitakazozumgumziwa ni pamoja na mchakato wa usajili wa jumuiya, uzinduzi wa nembo ya jumuiya, ripoti ya fedha pamoja na mipango ya jumuiya kwa mwaka 2014.

Tunaombwa kuzingatia muda wa kuanza kikao.

Asanteni,

David P. Semiono
Mwenyekiti
Tanzanite Society

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

ni matumaini kikao kilienda safi.:-)