Monday, April 22, 2013

Yokohama International Costume Parade
Matembezi ya 61 ya Kimataifa ya Mavazi ya Yokohama (Yokohama International Costume Parade)

Tunapenda kuwatangazia Watanzania wote kuwa matembezi ya kila mwaka ya Kimataifa ya Mavazi ambayo hufanyika katika jiji la Yokohama kwa lengo la kuhamasisha ushirikiano wa mataifa mbalimbali kupitia mila na desturi zao hasa mavazi yatafanyika tarehe 3 au 4 Mei 2013 kutegemea na hali ya hewa.

Matembezi yataanza saa 10:00 kuanzia Yamashita Park, kwa muda wa saa moja. Baada ya matembezi kutakuwa na chakula cha pamoja "Philippines Restaurent" Isesaki -cho.


Kwa ujumbe huu tunaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi ili kuendeleza ushikiano ambao umeanza kuimarika kati ya Tanzania na jiji la Yokohama. Ujumbe wa Tanzania katika matembezi haya utaongozwa na Mhe. Balozi Salome Sijaona. Ubalozi utashukuru kupokea majina ya watakaokuwa na nafasi ya kushiriki kupitia anuani zifuatazo:

tzrepjp@gol.com fmossongo@tanzaniaembassy.or.jp jmaleko@tanzaniaembassy.or.jp


Tangazo hili limetolewa na Ubalozi wa Tanzania
Tokyo, Japan
Tarehe 22.04.2013

No comments: