Wednesday, May 02, 2012

Tanzanite Society JP

MATEMBEZI YA HISANI (60TH YOKOHAMA INTERNATIONAL COSTUME PARADE, ALHAMISI TAREHE 3 MAY 2012
Ubalozi wa Tanzania nchini Japani unapenda kuwajulisha Watanzania wote waishio Tokyo, maeneo ya karibu na Tokyo na Japan kwa ujumla kuwa Mji wa Yokohama unaandaa matembezi ya Hisani (60th Yokohama International Costume Parade) tarehe 03/05/2012 au tarehe 04/05/2012 endapo kutakuwa na mvua tarehe 3.
Kwa mara ya kwanza maonyesho hayo yaliandaliwa na mji wa Yokohama mwaka 1953 kwa lengo la kuhamasisha jitihada za kufufua uchumi na utalii wa mji wa Yokohama kufuatia uharibifu ulitokana na Vita Kuu vya Pili vya Dunia (WWII). Kutoka kuasisiwa kwake maonyesho haya yamekuwa yakipata umaarufu mwaka hadi mwaka.
Katika matembezi ya mwaka 2012, Ubalozi umejulishwa na Kamati ya maandalizi kuwa Tanzania imechaguliwa na kuombwa kushiriki katika matembezi hayo. Maombi hayo yalifafanua zaidi kuwa Tanzania imechaguliwa na kuombwa kushiriki katika matembezi hayo kutokana na historia yake ya kupenda,kusimamia na kutetea amani, umoja na mshikamano duniani. 
Sababu nyingine ni kuwa Mji wa Yokahama una nia ya kuanzisha uhusiano (Sistercity Friendship) na mojawapo ya miji ya Tanzania katika siku za karibuni. Uhusiano ambao utajumuisha kupanda miti aina ya cherry blossom katika mji utakaochaguliwa Tanzania.
Hivyo matembezi hayo yanalenga pamoja na kuendeleza mshikamano wa watu wa Yokohama, yatatumika kuitangaza Tanzania, hususan mila na desturi za Mtanzania (amani, umoja na mshikamano).
Ili kuonyesha umoja na mshikamano wetu wa Tanzania, Ubalozi unapenda kuwaalika Watanzania wote waliopo Japan kujitokeza kwa wingi kushiriki matembezo hayo ya hisani. Aidha, katika kuainisha utamaduni wetu ni muhimu kuvaa mavazi ambayo yataelezea utanzania, mfano khanga kwa kina mama/dada na rubega kwa kina baba/kaka n.k.
Muda, Mahali na UmbaliMatembezi yatafunguliwa rasmi saa 4.45 (nne na dakika arobaini na tano) asubuhi mbele ya Hotel New Grand.
Matembezi hayo yatatanguliwa na matembezi ya watoto (Kid’s Parade) saa 4:45 (nne na dakika arobaini na tano) asubuhi, Yamashita Park-Red Brick Warehouse-Makutano ya Bankokubashi, ubali ni Km 1.4
Saa 5:15 (tano na robo) asubuhi, matembezi ya watu wazima (Super Parade) yataaza (Yamashita Park-Red Brick Warehouse- Bashamichi shopping avenue-Isesaki-cho 6 chome- umbali ni Km 3.4
Kwa wote watakaopenda kushiriki, tunaomba watume majina yao na mawasiliano yako kwenye barua pepe zifuatazo:tzrepjp@gol.com, fmossongo@tanzaniaembassy.or.jp jmaleko@tanzaniaembassy.or.jp
Ushiriki wa Tanzania katika matembezi hayo utaongozwa na Mhe. Salome T. Sijaona, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Japan.Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Tokyo, Japan

No comments: