Sunday, March 18, 2012

Taarifa ya Msiba

Ndungu WanaJumuiya na Wanatija,
Nasikitika kutoa taarifa ya msiba wa Baba Mzazi wa wanajumuiya na wanatija
wenzetu Abuu Njenga na Rashid Njenga (ambaye pia M/kiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Japan)
Msiba wa Baba yao Mzazi ulitokea usiku wa tarehe 14 March (alfajiri ya tarehe 15 kwa masaa ya Japan).
Ndugu zetu Abuu na Rashid sasa hivi wapo kwenye pilika pilika kwa maandalizi ya kurudi nyumbani
Tanzania kwa ajili ya kuwahi mazishi
Naomba tuungane kuwatakia wenzetu nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu sana kwao.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake l
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi
Kwa niaba ya Jumuiya ya watanzania wanaoshi nchini Japan

wenu
Bagilo Jumbe

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mwenyezi Mungu awatangulie..na awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu. Marehemu astarehe kwa amani amina.

Rachel siwa Isaac said...

Poleni sana Wafiwa na Mungu awape nguvu na uvumilivu katika wakati huu mgumu kwenu.

emu-three said...

Poleni sana, mungu ni muweza wakila jambo, na yeye ndiye wa kushukuruwa kwa kila jambo