KAMA OPTION

KAMA OPTION

KI

KI

eid

eid

Friday, November 25, 2011

Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, Ujerumani Hakuna kulala Mtu




Watanzania wanaoishi Ujerumani ! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru !
Kuanzia München hadi Berlin Chereko !Chereko !
FFU wa Ngoma Africa Band kutoa burudani ya kukata na Mundu !
Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!
Watanzania waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea miaka 50 ya uhuru
wa Tanzania bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona,sherehe hizo zinaanzia mjini
München siku ya 3 Dec 2011 ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za
Tanzania,mavazi,na mdahalo rasmi na usiku kutakuwa na muziki wa Ngoma Africa Band
katika mtaa wa Siebold Str,11 ndipo penye ukumbi.
Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio
mji mkuu wa Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi
wa UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja
huo unawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na
Bi.Tullalumba Mloge (katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin,
UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU !

No comments: