Tuesday, September 13, 2011

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO NCHINI JAPAN.

WATANZANIA TUISHIO JAPAN TUMESIKITISHWA SANA NA TAARIFA ZA MSIBA HUU MZITO KWA TAIFA LETU. MSIBA AMBAO UMESABABISHWA NA KUTOKEA KWA AJALI YA MELI YA MV SPICE, ILIYOTOKEA TAREHE 10/09/2011.

TUNAWASHUKURU SANA WALE WOTE WALIOONYESHA UJASIRI MKUBWA KATIKA ZOEZI LA UOKOAJI NA KUFANIKIWA KUASALIMISHA MAISHA YA WATANZANIA WENZETU KADHAA, NA PIA WALE AMBAO WAMEJITOLEA, NA WANAENDELEA KUJITOLEA KWA NAMNA MBALIMBALI ILI KUSAIDIA WALIONUSURIKA PAMOJA NA FAMILIA ZA WAFIWA.

TUNACHUKUA FURSA HII KUTOA POLE NA SALAMU ZETU ZA RAMBIRAMBI NA PIA KUWAHAKIKISHIA KUWA TUPO PAMOJA NANYI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAOMBOLEZO.

MWENYEZI MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU WOTE MAHALI PEMA PEPONI AMEN

JUMUIYA TA WATANZANIA WAISHIO NCHINI JAPAN

NJENGA, Rashid : MWENYEKITI
SUGAI, Prosper : MAKAMU MWENYEKITI

No comments: