Friday, May 20, 2011

Tanzanite SocietyNdugu watanzania wenzangu,
Kwa niaba ya Kamati ya kuandaa mkutano mdogo wa Watanzania kuchagua
viongozi wa kudumu.Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza nafasi
zitakazogombewa katika kipindi cha uchaguzi mdogo na sifa za mgombea.

1. Mwenyekiti wa Jumuiya
2. Makamu Mwenyekiti
3. Mweka Hazina
4. Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu

Kwa mujibu wa katiba kwa wale wote watakaopenda kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi ((1)~(4)), watatakiwa kuwa na sifa zifuatazo.

2. Kiongozi wa Jumuiya awe na sifa zifuatazo:
(a) Awe Mtanzania.
(b) Awe ameishi nchini Japani sio chini ya miezi sita na awe anategemewa kuishi
nchini Japani kwa zaidi ya mwaka mmoja.
(c)Awe na uwezo wa kumudu nafasi ya uongozi anayopewa.

Mkutano utafanyika katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania siku ya Jumapili, tarehe 22 mwezi Mei 2011
kuanzia saa 9 jioni. Anuani na ramani ya jinsi ya kufika ukumbi wa mkutano zilikwishatolewa katika matangazo yetu ya mwanzoni.

★ Ndugu watanzania wenzangu, Kwa wale wote watakaopenda kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi wanaruhusiwa kuanza kampeni. Mgombea anaruhusiwa kutumia
njia ya mtandao kufanya kampeni(Kijinadi)

Fomu ya uchaguzi na maelezo yake imeambatanishwa na inapaswa kujazwa na kurudishwa kwa katibu mkuu kabla ya Jumamosi na Fedha za kuchukua fomu zitumwe kwenye akaunti ya Jumuiya kabla ya Jumamosi 21/5/2011.

No comments: