Monday, February 14, 2011

we mama mbavu zanguBabu afurahishwa na style ya nywele ya mjukuu wake5 comments:

Mbele said...

Nimeipenda sana hii. Huwa nawatania waMarekani kuwa hawajui kucheka, nikifananisha na waAfrika, ambao tunapasuka mbavu kama anavyofanya huyu babu, hadi machozi kutiririka.

Halafu, wataalam wamethibisha kuwa kucheka kuna manufaa kiafya. Ni zoezi ambalo linaboresha ufanisi wa viungo kama mapafu na moyo na mzunguko wa damu mwilini. Msongamano wa mawazo unaoweza kudidimiza nafsi nao unapungua au kutoweka kwa kicheko.

Wa-Marekani wanaokuja Bongo, kwa mfano, wanashangaa kwa vipi nchi yenye dhiki namna hii watu wake wanaonekana wana furaha kuliko wa-Marekani. Mimi huwa nawatania kuwa jawabu ni vile vijiwe vyetu ambamo tunapiga stori na michapo :-)

mumyhery said...

hahaha umenikumbusha vijiwe vya bongo Shukran Mkuu

Swahili na Waswahili said...

hahhahaa imebidi nami nicheke tuu!

SIMON KITURURU said...

:-)

PASSION4FASHION.TZ said...

Inachekesha,naona na mimi kaniambukiza nimejikuta nacheka kama yeye.