Wednesday, December 15, 2010

Sherehe ya Miaka 49 ya Uhuru yafana JapanMzee Sijaona, Mheshimiwa Balozi Mama S. Sijaona na Mkurugenzi wa Kampuni ya Brilliant Auto & General Trading Bw R. Njenga


Waungwana.

Naomba kutoa pongezi binafsi kwenda kwa Jumuiya Ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japan.
Kwa kufanikisha sherehe za Uhuru zilizofanyika jana (12.December.2010) kwenye ukumbi
wa PPP hapo Sagamino, Kanagawa.Mheshimiwa Balozi S. Sijaona akikata keki ya Uhuru

Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Balozi Mrs. Salome Sijaona.
Ambaye kwenye hotuba yake aliongela mambo mengi, ikiwemo kusisitiza Umoja miongoni
mwa Watanzania wanaoishi nchini Japan. Na pia kuwakumbusha majukumu yao katika kuleta maendeleo ya
Tanzania ambayo sasa imetimiza miaka 49 kwa upande wa Tanganyika.

Pia mgeni rasmi alifungua rasmi tovuti hii ya Jumuiya ijulikanayo kwa jina la:
http://www.tanzanitesociety.jp
Watanzania wote mnaruhusiwa kujiunga nayo kwa kutembelea tovuti ifuatayo:
http://www.tanzanitesociety.jp/ForumMemberProfile/register
ambapo utafanya Registration. Ili kuweza kushiriki katika majadiliano mbalimbali.

Ni matumaini ya Jumuiya kuwa Watanzania wote wanaoishi nchini Japan watajiunga na Jumuiya
na kuwa wanachama hai. Baada ya registration, Administrator atakuwa na jukumu la
kutofautisha wale ambao wamekishwajiunga na Jumuiya na wale ambao bado hawajafanya hivyo.

Katika Risala ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Balozi,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japan (Tanzanite Society),
Dr. Ally Y. Simba, Alisisitiza siku hiyo iwe ya kusherehekea Uhuru wa Tanganyika na
Zanzibar na sio upande mmoja tuu.

Mwenyekiti wa Jumuiya pia alichukua muda kuwashukuru wengi waliojitokeza kuchangia kwa hali na mali
utayarishaji wa Sherehe hiyo wakiwemo wafuatao:
Mkurugenzi wa Noba International Bw Jumbe Bagilo na Mkurugenzi wa Rosper International Bw Prosper Sugai wakiwa pamoja na Wakili Kijima

<1> Mkurugenzi wa Rosper International, Nd. Prosper Sugai,Bi Asmah Kobayashi akiteta na Mwakilishi toka ubalozi wa Kenya<2>Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya Bi Asmah Kobayashi,<3>Mkurugenzi wa Noba International Nd. Bagilo Jumbe, naMkurugenzi wa Kampuni ya Brilliant Auto and General Trading Bw Rashid Njenga


<4>Mkurugenzi wa kampuni ya Brilliant Auto and General Trading, Nd. Rashid Njenga.

Afisa Ubalozi Mama Kavishe mwenye suti nyeupeAfisa Ubalozi Mama Maleko mwenye mnyamaAfisa Ubalozi Bw Musongo akiitayarisha kumsindikiza Balozi


Pia shukrani nyingi zilienda kwa ubalozi wetu kwa ushirikiano na kwa mchango wao wa hali na mali.


Risala Nzima ya Mwenyekiti inapatikana hapa:

http://www.tanzanitesociety.jp/news/show/32/Sherehe ilikuwa na mambo mengi mazuri kuanzia kwenye Muziki ambapo Tanzanite Band walitumbuiza.DJ Zee alileta burudani yenye kifani. Mr. Daima pia hakusisita kutoa tumbuizo la kutosha.

Kwenye suala zima la chakula Da' Upendo Mwimbage, Da' Mariam Yazawa na Da' Anna Magugudi

hawakufanya ajizi kwenye kuandaa chakula chenye hadhi ya juu mno.

Administrator,
Tanzanite Society.