Sunday, November 28, 2010

SHEREHE YA MIAKA 49 YA UHURU

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani inapenda kuwataarifu ya kuwa inaandaa tafrija ya kusherekea siku ya uhuru.

Mheshimiwa Balozi Mama Salome Sijaona atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hii.

Sherehe hii itafanyika siku ya tarehe 12/12/2010 (Jumapili), kuanzia saa Nane mchana mpaka saa saa Tatu usiku katika ukumbi wa club ya PPP uliopo karibu station ya Sagamino (sotetsu line). Ukifika station ya Sagamino tokea SOUTH EXIT. Ni dakika 5 kutokea station. Anuani ya ukumbi ni: Ebina-shi, Higashiwagaya 5-1-15. Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kufika ukumbini piga namba zifuatazo: 080- 1326-9700, 080-3242-7442.
Ingawa shughuli hii inaandaliwa na Jumuiya, Watanzania wote wanakaribishwa kuhudhuria pamoja na familia na marafiki zao.

Tungependa siku hiyo itumike kuwakutanisha watanzania ili nao waweze kubadirishana mawazo na kufahamiana ili kuweza kujenga umoja wenye nguvu zaidi na kutafakari mustakabali wa nchi yetu tangu ipate uhuru. Pamoja na hayo, kutakuwa na uzinduzi rasmi wa Tovuti ya Jumuiya na kutakuwa mjadala wa mada mbili tatu zitakazotolewa na watu mbalimbali, bila kusahau muziki wa Kitanzania.

Ili kurahisisha shughuli za maandalizi hasa vyakula na vinywaji, tafadhali tunaomba wale wote watakaotaka kuhudhuria tafrija hii kuthibitisha kwa kujiandikisha wao na wale watakaofutana nao kwa viongozi wafuatao:

1. Upendo Mwimbage: 080- 4002-9700
2. Mariam Yazawa: 090-4422- 8555
3. Gwakisa Muhoka: 080-3242-7442
4. Bagilo Jumbe: 090-1733- 7447
5. Juma Kipaya: 080-3414- 4460
6. Amani Paul: mail: amani.paul@gmail.com, simu: 080-4200- 0684
7. Christopher Ntyangiri: email: ntyangiri2@yahoo.com, simu: 090-9377-3524
8. Asmah Kobayashi: 080-3311-8183
9. Bw Yusuf Mzee wa MAJI: 080-2064-6573

Siku ya mwisho ya kujiandikisha ni tarehe 4/12/2010. Wasiojiandikisha na kuthibitisha kuhudhuria hawataruhusiwa kuingia ukumbini siku ya tafrija. Pia tunawaomba wale wote watakaohudhuria kuzingatia muda.

Tafadhali ukipata taarifa muhabarishe Mtanzania mwenzako.

Ahsanteni.
Ally Y. Simba,
Mwenyekiti,
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani

1 comment: