Saturday, October 30, 2010

TANZANITE SOCIETY JP

Ndugu Wanajumuiya na Watanzania wote kwa ujumla,

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani unapenda kuwatangazia kuwa kutakuwepo na Mkutano Mkuu wa Mwaka kwa wanajumuiya wote na Watanzania wote ambao wataweza kufika katika Ukumbi wa Odakyu Sagamihara kama ifuatavyo :

Tarehe: 21/11/2010
Mahala: Odasaga Plaza
Muda: Kuanzia saa 12:15 jioni

Agenda zitatangazwa baadae.

Naomba uongozi wote kwa ujumla tusaidiane kuwafahamisha wanajumuiya wote na wale ambao hawajafanya juhudi za kujiunga na jumuiya kuhusu mkutano huu muhimu.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Jullius L. Mwombeki Jnr
Katibu Mkuu -
Jumuiya ya WaTanzania Wanaoishi nchini Japani