Monday, October 04, 2010

Chombo cha Ushahidi‏


Vijana FM inatumia Crowdmap, chombo kilichotengenezwa na Ushahidi, kukusanya taarifa, mawazo na uzoefu wakati wa Uchaguzi Mkuu Tanzania. Ni matarajio yetu kwamba chombo hiki kitawapa jukwaa watu kutoa taarifa, maoni, kuanzisha mijadala na kueneza ujuzi wa mchakato wa uchaguzi na matukio mbalimbali.

Taarifa zinaweza kuwasilishwa kwa njia tatu:
Kwa kutuma barua pepe: TZelect (at) gmail (dot) com
Kwa Twitter hashtags #TZelect au #uchaguzitz (Shukrani Jamii Forums)
Kwa kujaza fomu kwenye tovuti

1 comment:

emu-three said...

Ahsante, angalau kidogokidogo watu wanaanza kugundua umuhimu wa `taarifa sahihi'. Vyombo kama hivi vitasiada , ingawaje `mchakachuo wa kura' bado haujagundulika njia ya kuudhibiti!