Tuesday, August 31, 2010

Futari

Boga la Nazi
Vipimo:

Boga 1
Tui La Nazi 2 Vikombe
Sukari 1 kikombe
Hiliki 1/2 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha na Kupika
1. Unamenya maboga kiasi ukipendacho.
2. Unayakata kata vipande vidogo vidogo.
3. Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika.
4. Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.
5. Kisha unamimina tui la nazi.
6. Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Yaani Da´M umenikumbusha mbali kweli boga mmmhh hapa mate yanadondoka si mchezo.

chib said...

Natamani kuila hiyo picha.

emu-three said...

Ahsante kwa kutupa hii, safi sana kwa futari, nitamwambia mama nanihii aitayarishe angalau leo